Rais wa Tanzania atoa wito wa juhudi zaidi za kupambana na maambukizi mapya ya UKIMWI
2022-12-02 11:28:56| CRI

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ametoa wito kwa wadau wa mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI kuendeleza juhudi zao ili kuzuia maambukizi mapya.

Akihutubia taifa kuadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani, Rais Hassan amesema kuwa lengo muhimu ni kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030 kama mpango ulivyotangazwa na Shirika la kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS).

Kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mkoani Lindi, Rais Samia amesema ni muhimu sana kuyalinda makundi yaliyo hatarini, hasa vijana wenye umri kati ya miaka 15 na 24, ili kuwaepusha na maambukizi.