Shenzhou No.14 yarudi duniani baada ya kumaliza kazi angani
2022-12-05 11:08:28| cri

Chombo cha safari ya anga ya juu cha kubebea watu Shenzhou No.14 kimetua duniani kwa mafanikio baada ya kumaliza kazi kwenye anga ya juu. Wanaanga wakiwemo Chen Dong, Liu Yang na Cai Xuzhe wamethibitishwa kuwa na hali na afya nzuri.

Chombo hicho kikibeba wanaanga hao watatu kilirushwa angani tarehe 5 Mei, na kuunganishwa na moduli kuu ya Tianhe ya Kituo cha Anga ya Juu ya Tiangong. Katika miezi 6 iliyopita, wanaanga hao walifanya majaribio mbalimbali ya kisayansi na kiteknolojia, kuandaa darasa la angani kwa wanafunzi walio duniani, na kutoka nje mara tatu ili kuunda na kurekebisha vifaa.

Chen amekuwa mwanaanga wa kwanza wa China kukaa kwenye anga ya juu kwa zaidi ya siku 200.