Jeshi la Mali laangamiza magaidi 66 katika mwezi Novemba
2022-12-05 11:12:42| cri

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Mali (Dirpa) imesema, jeshi hilo limewaua magaidi 66 katika mwezi Novemba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Dirpa, katika operesheni zilizofanywa mwezi Novemba, jeshi la Mali limeteketeza vituo vingi vya magaidi, kukamata au kuharibu magari, silaha na vifaa vingine, huku likikamata mifugo na nafaka zilizoibwa.

Tangu mwaka 2012, Mali inakabiliwa na migoro mbalimbali ikiwemo usalama, siasa na uchumi. Uasi wa uhuru, uvamizi wa wanajihadi na ghasia kati ya jamii mbalimbali zimesababisha vifo vya maelfu ya watu, na wengine wengi kukimbia makazi yao katika nchi hiyo.