Rais wa Zimbabwe ahimiza taifa kukabiliana na upungufu wa nishati
2022-12-05 11:10:19| cri

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametoa wito kwa nchi nzima kuchukua hatua za kukabiliana na upungufu wa nishati unaoikumba nchi hiyo, ikiwemo kuongeza uagizaji na matumizi ya nishati safi.

Rais Mnangagwa ametoa wito huo kupitia chapisho lake linalotolewa kila wiki kwenye gazeti la serikali, Suday Mail. Amesema utoaji wa nishati nchini Zimbabwe umepungua kwa kiasi kikubwa baada ya kituo kikuu cha Kariba kinachozalisha umeme kwa nishati ya maji, kupunguza uzalishaji wake kwa nusu kutokana na kupungua kwa kiwango cha maji.

Rais Mnangagwa amesema, serikali yake itatafuta haraka ufumbuzi wa upungufu wa nishati. Ameongeza kuwa wanahitaji kuziba pengo la hivi sasa kupitia kuongeza manunuzi kutoka nje, na ni lazima kuhamasisha rasilimali za kutosha ili kutimiza lengo hilo.