Mwili wa Jiang Zemin wachomwa Beijing
2022-12-05 17:06:28| cri

Mwili wa rais wa zamani wa China Hayati Jiang Zemin umechomwa moto leo mjini Beijing. Rais Xi Jinping wa China, akiongozana na aliyekuwa rais wa China Hu Jintao na viongozi wengine wa Chama na serikali walitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Jiang katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China, na pia kusindikiza mwili kwa ajili ya kuchomwa katika Makaburi ya Mapinduzi ya Babaoshan.