Sudan yasaini makubaliano ya muongozo wa kumaliza mkwamo wa kisiasa
2022-12-06 09:46:35| CRI

Viongozi wa kijeshi na kiraia nchini Sudan wamesaini makubaliano ya muongozo wa kisiasa ili kumaliza mkwamo wa kisiasa na kuanzisha mamlaka ya mpito ya kiraia kwa miaka miwili.

Kamanda wa jeshi la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan na kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka Mohamed Hamdan Dagalo walisaini makubaliano jana Jumatatu kwa niaba ya vikosi vya kijeshi. Wakati huohuo wawakilishi wa Muungano wa vikosi vya Uhuru na mabadiliko, Revolutionary Front, mashirika mengine ya kisiasa, vyama vya wafanyakazi na asasi za kiraia walisaini kwa niaba ya makundi ya kisiasa.

Makubaliano hayo yanaamua vyombo vinne vya mamlaka ya mpito, vikiwemno baraza la kisheria na mabaraza ya mahakama pamoja na tume huru.

Aidha kwa mujibu wa makubaliano, pande zinazosaini azimio la kisasa, kupitia mashauriano, ndio zitachagua baraza la utawala wa kiraia lenye ukomo maalumu ili kuwakilisha mkuu wa nchi na kuwa alama ya utawala, huku zikijadiliana kuchagua waziri mkuu ambaye ataunda baraza la mawaziri.