Cameroon kuimarisha usalama mwisho wa mwaka
2022-12-06 09:51:25| CRI

Waziri wa ulinzi wa Cameroon Bw. Joseph Beti Assomo jana alisema jeshi na askari wa Cameroon wamefanya maandalizi ya kuweka hali ya utulivu na kutokuwa na vizuizi kote nchini wakati watu wakisherehekea sikukuu ya Christmas na mwaka mpya.

Assomo alisema siku kuu hizi zinafanya watu wengi kwenda huku na kule, hivyo vikosi vya usalama vinapaswa viwe macho zaidi ili kuhakikisha amani.

Assomo alipohudhuria mkutano wa usalama uliofanyika mjini Yaounde alisema Kombe la Dunia linalofanyika Qatar linachochea hali ya uchangamfu wa watu.