Timu ya madaktari wa China nchini Tunisia wapongezwa kwa huduma zao
2022-12-06 09:52:31| CRI

Waziri wa Afya wa Tunisia Ali Mrabet amekutana na timu ya 26 ya madaktari wa China nchini Tunisia, na kuwapongeza kwa kutoa huduma ya kipekee kwa watu wa nchi hiyo.

Katika hafla ya kuipongeza timu hiyo inayomaliza muda wake, Mrabet amesema watu wote wa timu hiyo walishikilia kuendelea na kazi zao wakati wa janga la COVID-19, na kutoa mchango mkubwa kwa afya ya Watunisia.

China imetuma wahudumu wa afya zaidi ya 1,100 nchini Tunisia katika takriban miaka 50 iliyopita. Waziri huyo amebainisha kuwa, utendaji bora wa madaktari wa China unaonesha kiini cha ushirikiano wa afya kati ya Tunisia na China.

Mkuu wa timu ya madaktari wa China Xu Chuyang amesema, madaktari wa timu hiyo daima wanaamini kwamba madaktari hawana mipaka, maisha ya watu ndio ya kwanza, na ni lazima wafanye juhudi zote kumtibu kila mgonjwa.