Kongamano la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China na Nchi za Kiarabu la Mwaka 2022 lafanyika Saudi Arabia
2022-12-07 15:04:41| cri

Kongamano la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China na Nchi za Kiarabu la mwaka 2022 limefanyika jana mjini Riyadh, Saudi Arabia.

Kongamano hilo limeandaliwa kwa pamoja na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na Wizara ya Habari ya Saudi Arabia, chini ya kauli mbiu ya "Kuimarisha mawasiliano na kufunzana: Kukuza ujenzi wa jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye mustakabali wa pamoja." Maafisa wa serikali, wawakilishi wa vyombo vya habari pamoja na wataalamu na wasomi wapatao 150 kutoka China na nchi 22 za Kiarabu wamehudhuria kongamano hilo kwa njia ya mtandao au moja kwa moja.

Katika hotuba yake kwa njia ya video, Waziri wa Biashara ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Habari wa Saudi Arabia Majid bin Abdullah Al-Qasabi alisema nchi za Kiarabu zinaichukulia China kama mshirika wa kutegemewa wa maendeleo ya pamoja katika nyanja mbalimbali, na zinatarajia kuwa pande hizo mbili zitaimarisha mawasiliano ya kitamaduni kupitia kongamano hilo, kukuza maelewano kati ya watu na watu, na kuhimiza upatikanaji wa maendeleo katika nyanja mbalimbali. Pia ametoa wito kwa vyombo vya habari vya nchi za Kiarabu na China kutekeleza kikamilifu matokeo ya kongamano hilo na kuendelea kusaidia ushirikiano wa nchi za Kiarabu na China.

Mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) Shen Haixiong katika hotuba yake kwa njia ya video, alisema Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China uliomalizika muda si mrefu uliopita, umetia msukumo mkubwa katika ushirikiano wa kirafiki kati ya China na nchi nyingine mbalimbali, na kukuza maadili ya kawaida ya binadamu wote. Amesema CMG italichukulia kongamano hilo kama fursa ya kuzidisha mawasiliano na majadiliano na sekta zote za jamii katika nchi za Kiarabu, kuimarisha ushirikiano wa kivitendo, na kutekeleza kikamilifu Pendekezo la Maendeleo Duniani na Pendekezo la Usalama Duniani. Pia kusaidia kwa pamoja uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Nchi za Kiarabu kufikia kwenye kiwango cha juu zaidi na kuchangia nguvu ya vyombo vya habari, ili kukuza ujenzi wa jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya, na ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Kama moja ya mafanikio muhimu ya kongamano hilo, CMG na Umoja wa Utangazaji wa Nchi za Kiarabu kwa pamoja wametoa "Pendekezo la Kukuza Mawasiliano na Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China na Nchi za Kiarabu", na kuhimiza vyombo vya habari vya China na nchi za Kiarabu kuimarisha kufundishana, kuzingatia majukumu ya vyombo vya habari, na kuimarisha ushirikiano na mawasiliano ili kutoa michango ya vyombo vya habari katika kukuza zaidi uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa China na nchi za Kiarabu.