Wasomali zaidi ya elfu 80 wakimbilia Kenya kutokana na ukame
2022-12-07 09:24:32| CRI

Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema, watu zaidi ya elfu 80 wamewasili kwenye kambi za wakimbizi za Dadaab zilizoko kaskazini mashariki mwa Kenya kutokana na hali isiyo salama inayoendelea na ukame mkali.

Shirika hilo limetoa taarifa ikisema, wengi wa wakimbizi hao waliwasili katika miaka miwili iliyopita. Na kusisitiza kuwa msaada mkubwa unahitajika sio tu nchini Kenya, bali pia nchini Somalia na Ethiopia, ambako mamilioni ya watu wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu, wakati mvua zikiendelea kukosekana.

Ingawa hivi karibu idadi ya wakimbizi wanaofika inapungua, UNHCR na wenzake wamekadiria kuwa watu wapatao elfu 24 wamewasili tangu mwishoni mwa Septemba.