Uongozi wa CPC wajadili kazi za kiuchumi za mwaka ujao na mapambano dhidi ya ufisadi
2022-12-07 12:04:11| cri

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imeitisha mkutano jana Jumanne ili kuchambua na kujadili kazi za kiuchumi kwa mwaka 2023 na kufanya maandalizi ya kuboresha mwenendo na uadilifu wa kimaadili wa Chama na kupambana na ufisadi.

Mkutano huo uliendeshwa na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping.