Mafunzo ya ufundi stadi kushika nafasi ya juu katika sera mpya ya elimu nchini Tanzania
2022-12-07 09:26:53| CRI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Tanzania Adolf Mkenda amesema sera iliyopitiwa upya ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 imetoa umuhimu kwa mafunzo ya ufundi stadi, na kwamba mapitio ya sera hiyo pamoja na mitaala ili kuimarisha ubora wa elimu nchini humo yamekamilika.

Akiongea kwenye mkutano wa wadau wa elimu na washirika wa maendeleo mjini Dodoma, Mkenda alibainisha kuwa maoni ya wadau kuhusu umuhimu wa kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi katika sera mpya ya elimu itakayozinduliwa baadaye yamezingatiwa kwa umakini. Amesema mafunzo ya ufundi stadi ni muhimu katika kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mchakato huo wa mapitio ya sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 na mitaala ulianza kufuatia maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan alipohutubia bunge mwaka 2021.