Maafisa wa Pembe ya Afrika wasisitiza kudumisha amani na utulivu wa kikanda
2022-12-07 09:28:21| CRI

Maafisa waandamizi wa nchi za eneo la Pembe ya Afrika wamesema, eneo hilo limejishughulisha na kukuza amani, utulivu, na ukuaji shirikishi baada ya vita na mizozo ya kiikolojia vilivyoendelea kwa miongo kadhaa.

Wakizungumza katika kongamano la mtandaoni lililoitishwa na Jopo la Washauri Bingwa Brookings, maafisa hao wamesema kukabiliana na vitisho vya usalama na mazingira ni kiini cha juhudi za kuchochea ukuaji wa uchumi na mshikamano katika eno hilo.

Waziri wa Sheria wa Ethiopia Gedion Timothewos amesema eneo la Pembe ya Afrika limekumbwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe, ukame, uhamiaji wa kulazimishwa na ugaidi, na utatuzi wa changamoto hizo wa muda mrefu unategemea kuimarisha dhamira ya kisiasa, ushirikiano wa kikanda, na ushiriki wa raia.

Monica Juma ambaye ni mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Rais William Ruto wa Kenya, amesema serikali ya Kenya inaunga mkono juhudi za kikanda zinazolenga kukabiliana na migogoro, misimamo mikali, majanga ya asili na ukosefu wa maendeleo katika eneo hilo.