Kamati Kuu ya CPC yaitisha mkutano kuhusu hali ya uchumi
2022-12-08 15:09:40| cri

Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imeitisha mkutano uliowakutanisha wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya kidemokrasia, viongozi wa shirikisho la viwanda na biashara, na wawakilishi wasio na chama, ili kusikiliza maoni na mapendekezo yao kuhusu hali ya uchumi kwa mwaka huu, na kazi za kiuchumi kwa mwaka ujao.

Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping ameendesha mkutano huo na kutoa hotuba akisema, mwaka ujao utakuwa mwaka wa kwanza kutekeleza kikamilifu mipango iliyowekwa katika Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, na kazi za kiuchumi zinapaswa kuzingatia kanuni za uthabiti na kutafuta maendeleo kwa utulivu, na kutekeleza kikamilifu dhana mpya ya maendeleo, ili kuweka mwanzo mzuri wa ujenzi wa ujamaa wa kisasa katika pande zote.