Msomi wa Cameroon: Uungaji mkono wa China kwa Umoja wa Afrika kujiunga na G20 unatia moyo
2022-12-08 09:12:16| CRI

Natumaini u mzima buheri wa afya msikilizaji na karibu sana kwenye kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kila jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Katika kipindi cha leo msikilizaji, pamoja na habari mbalimbali kuhusu China na nchi za Afrika, tutakuwa na ripoti itakayozungumzia nia ya Afrika ya kujiunga na Kundi la Nchi 20 (G20). Pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi kuhusu hafla ya kusherehekea Opera ya Kichina iliyofanyika katika Ukumbi wa Kitaifa wa Sanaa jijini Nairobi nchini Kenya.