Makampuni ya China yakabidhi bwawa la kuogelea lililokarabatiwa nchini Zimbabwe
2022-12-08 09:33:53| CRI

Kundi la makampuni ya China lililoko Zimbabwe jana lilikabidhi bwawa la kuogelea lililokarabatiwa mjini Harare, ambalo linatarajiwa kuhimiza maendeleo ya michezo ya watu, na kuwaepusha vijana kujihusisha na dawa za kulevya.

Mradi huo wa ukarabati ulifadhiliwa na Shirikisho la makampuni ya China nchini Zimbabwe (CCEZ), ambalo ni la biashara linaloundwa na makampuni 80 ya China huko Zimbabwe, pia linaunga mkono miradi ya hisani nchini humo.

Naibu Mwenyekiti wa CCEZ Bibi Liu Baixue alisema mradi huo utafanya kazi muhimu katika kukidhi mahitaji ya burudani ya watu na kuwalinda vijana.

Kwa upande wa meya wa Harare Bw. Jacob Mafume aliishukuru CCEZ kwa kukarabati bwawa hilo la kuogelea, akisema kitendo hicho ni mfano wa kutekeleza wajibu wa jamii.