UM yasema usafirishaji haramu wa mali za kiutamaduni umeharibu utambulisho wa Afrika
2022-12-08 09:35:26| CRI

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limesema, usafirishaji haramu wa mali za kiutamaduni umeharibu utambulisho wa Afrika.

Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika hilo Bw. Hubert Gijzen amesema katika hotuba yake iliyosomwa na mshauri wa kikanda wa mawasiliano na habari wa Afrika katika shirika hilo Bi Misako Ito, kwamba usafirishaji haramu wa vitu halisi vya kiutamaduni umekuwepo katika historia nzima ya bara hilo kwa mitindo na madhumuni tofauti.

Akiongea kwenye warsha ya kupambana na usafirishaji haramu wa mali za kiutamaduni katika Afrika Mashariki iliyofanyika huko Nairobi, Kenya Bi Ito amesema, usafirishaji huo haramu kwa muda mrefu umekuwa ukitishia utambulisho, historia na kumbukumbu za watu wa Afrika.

Bi Ito ametoa mwito kwa wadau wote kujiunga na juhudi ya kulinda urithi wa Afrika kwani unawakilisha vyombo maalumu vya diplomasia za utamaduni.