Mapendekezo ya China yapata uungaji mkono mwingi wa Jumuiya ya Kimataifa
2022-12-09 09:29:48| CRI

Wakati rais Xi Jinping wa China akihudhuria mkutano wa kwanza wa kilele wa China na nchi za Kiarabu na mkutano wa kilele wa kamati ya ushirikiano kati ya China na nchi za Kiarabu za ghuba, na kufanya ziara nchini Saudi Arabia, Jopo la Washauri Bingwa la Chaneli ya CGTN ya Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG likishirikiana na Kituo cha vyombo vya habari vya kimataifa na mawasiliano cha Tsinghua-Epstein limefanya uchunguzi wa maoni unaowashirikisha wahojiwa elfu 4 kutoka nchi 20 duniani. Uchunguzi huo umeonesha kuwa asilimia 94.2 ya wahojiwa wanapongeza pendekezo la thamani ya pamoja ya binadamu wote ya “Amani, Maendeleo, Usawa, Haki, Demokrasia na Uhuru” lililotolewa na China, huku asilimia 85 ya wahojiwa wakipongeza wazo la “Jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu”.

Katika miaka kumi iliyopita, China imesaini nyaraka za ushirikiano za kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na nchi 20 za kiarabu, ambapo nchi 17 za kiarabu zinaunga mkono pendekezo la maendeleo ya dunia lililotolewa na China. Kote duniani, asilimia 78.4 ya wahojiwa wanakubali pendekezo la maendeleo ya dunia, huku wakiona kuwa maendeleo ni njia muhimu ya kutatua masuala ya dunia. Asilimia 79.4 ya wahojiwa wamepongeza matunda ya ushirikiano ya kikundi cha marafiki wa pendekezo la maendeleo ya dunia kinachoshirikiana na China, huku wakiona kuwa nchi zinazoongoza kwa nguvu za kitaifa zinatakiwa kutekeleza majukumu ya kimataifa yanayolingana na hadhi zao.

Wakati dunia ikikabiliwa na mabadiliyo ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika miaka mia moja iliyopita, China na nchi za kiarabu zote zinakabiliana na majukumu ya kihistoria ya kustawisha taifa na kuharakisha maendeleo ya nchi. Katika uchunguzi huo, asilimia 85.2 ya wahojiwa wanaona kuwa nchi mbalimbali zinatakiwa kuchukua hatua kukabiliana kwa pamoja na changamoto na hatari za maendeleo ya dunia. Asilimia 84.7 ya wahojiwa wanatarajia nchi mbalimbali kuhimiza kufikiwa kwa maendeleo ya dunia yanayoweza kuhimili na ya aina nyingi na kulinda pamoja utulivu wa uchumi wa dunia. Mbali na hayo, asilimia 84.1 ya wahojiwa wanaona kuwa msingi wa ushirikiano ni kuheshimu njia na mifumo tofauti ya maendeleo ya nchi mbalimbali, huku asilimia 89.6 wakitaka nchi mbalimbali kutatua migongano ya kimataifa kupitia mazungumzo.