Uchumi wa Kenya wakadiriwa kukua kwa asilimia 5.5 mwaka 2022
2022-12-09 09:33:01| CRI

Ripoti mpya iliyotolewa na Benki ya Dunia imesema uchumi wa Kenya unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.5 mwaka 2022, kutoka asilimia 7.5 mwaka 2021.

Ripoti hiyo mpya iliyotolewa jana kuhusu Taarifa Mpya ya Uchumi wa Kenya imesema kupanuka kwa uchumi kutakuwa chachu ya ongezeko kubwa la huduma na viwanda licha ya utendaji duni wa sekta ya kilimo. Matarajio ya ukuaji wa Kenya yanasalia kuwa mazuri, hata hivyo, athari zinazojitokeza zinaleta changamoto kwenye ufufukaji mkubwa.

Ripoti hiyo inayotolewa mara mbili kwa mwaka hutathmini maendeleo na matarajio mapya ya kiuchumi na kijamii nchini Kenya na kuyaweka katika muktadha wa muda mrefu na wa kimataifa.