Rais Xi asema China itaiunga mkono na kusaidia Somalia katika ujenzi upya na kupambana na ugaidi
2022-12-09 20:38:32| cri

Rais Xi Jinping wa China amesema China iko tayari kutoa msaada kadiri iwezavyo kwa ajili ya ujenzi mpya na maendeleo ya kijamii na kiuchumi wa Somalia, na kuhimiza makampuni ya nchi hizo mbili kutafuta ushirikiano katika maeneo ya kilimo, uvuvi na afya.

Rais Xi amesema hayo mjini Riyadh Saudi Arabia alipokutana na Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, na kuongeza kuwa China inaunga mkono serikali ya Somalia katika kuimarisha uwezo wake wa kudumisha utulivu na mapambano dhidi ya ugaidi.