Xi atunukiwa shahada ya heshima ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha King Saud
2022-12-09 09:28:42| CRI

Rais Xi Jinping wa China Alhamisi alihudhuria hafla ya kutunuku shahada ya heshima ya udaktari ya Chuo Kikuu cha King Saud kwenye kasri la kifalme mjini Riyadh, ambapo Mwanamfalme wa Saudia na Waziri Mkuu Mohammed bin Salman Al Saud pia alihudhuria hafla hiyo.

Hafla hiyo iliongozwa na rais wa Chuo Kikuu cha King Saud, Badran bin Abdulrahman Al-Omar, ambapo Waziri wa Elimu wa Saudi Arabia Yousef bin Abdullah Al-Benyan alimkabidhi Xi cheti cha shahada ya heshima ya udaktari.

Ikibainisha kuwa Chuo Kikuu cha King Saud ni cha kwanza cha Saudi Arabia ambacho nchi hiyo inajivunia, Saudia ilisema kuwa China imebeba jukumu muhimu katika muundo wa uchumi wa dunia na ni mfano wa kuigwa kwa watu wa nchi zote wanaotamani maendeleo na ustawi, na kuongeza kuwa mafanikio makubwa ya China yanachangiwa na kuwa na kiongozi mkuu kama Xi, ambaye ana dira ya kimkakati na ya muda mrefu.