Rais wa China azungumza na waziri mkuu wa Saudi Arabia
2022-12-09 09:32:16| CRI

Rais Xi Jinping wa China ambaye yuko ziarani nchini Saudi Arabia amezungumza na mrithi wa mfalme wa Saudia Mohammed bin Salman, ambaye pia ni waziri mkuu wa nchi hiyo.

Rais Xi amebainisha kuwa Saudia ni nchi muhimu ya Kiarabu na Kiislamu, ni nguvu huria muhimu ya dunia yenye ncha nyingi, na pia ni mwenzi muhimu wa kimkakati wa China katika kanda ya Mashariki ya Kati. Amesema katika miaka ya hivi karibuni, China na Saudia zimedumisha maendeleo ya kwango cha juu ya uhusiano, ambao umekuwa muhimu zaidi kufuatia utatanishi wa hali ya kimataifa na ya kikanda ya hivi leo. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Saudia katika njia ya kujistawisha, kuendeleza uratibu wa kimkakati, kukuza ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kuimarisha mawasiliano katika mambo ya kimataifa na ya kikanda, ili kuhimiza uhusiano wao wa wenzi wa kimkakati katika pande zote kupata maendeleo zaidi.

Mohammed amesema uhusiano kati ya Saudi Arabia na China ni wa karibu na wa kirafiki, na katika kanda ya Mashariki ya Kati, Saudia ni mwenzi wa China katika ushirikiano wa kimkakati wa pande zote. Ameongeza kuwa Saudia inapenda kuongeza nguvu ya kusaidiana na China, na kushughulikia kwa pamoja kuinua zaidi kiwango cha uhusiano wao wa wenzi wa kimkakati katika pande zote.