Rais wa China asema China inaunga mkono njia ya mendeleo ya Tunisia
2022-12-09 16:17:21| cri

Rais wa China Xi Jinping amesema China inaiunga mkono Tunisia kwa kuchagua njia yake ya kuleta maendeleo kuendana na mazingira ya taifa hilo, na ameeleza kupinga nchi za kigeni kuingilia kati mambo ya ndani ya Tunisia.

Rais Xi amesema hayo alipokutana na mwenzake wa Tunisia, Kais Saied katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.