Majivu ya Hayati Jiang Zemin yatawanywa baharini
2022-12-12 08:52:25| CRI

Majivu ya Hayati Jiang Zemin yametawanywa baharini kupitia mlango wa Mto Yangtze Jumapili, kufuatia matakwa ya Hayati Jiang na familia yake.   

Jiang alifariki mjini Shanghai tarehe 30 Novemba, akiwa na umri wa miaka 96, na mwili yake kuchomwa tarehe 5 Desemba mjini Beijing.

Cai Qi, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na mjumbe wa Sektretarieti ya Kamati Kuu ya CPC na maofisa wengine, mke wa marehemu Bibi Wang Yaping, na wanafamilia walishiriki katika hafla hiyo.