Palestina yalaani shinikizo la Marekani kwa UM kuhusu kutotengeneza upya orodha ya kampuni zake katika makazi ya Waisraeli
2022-12-12 08:55:04| CRI

Palestina jana imelaani hatua ya Marekani ya kuushinikiza Umoja wa Mataifa kuhusu kutotengeneza upya orodha ya kampuni za nchi hiyo zinazofanya kazi katika makaazi ya waisraeli kwenye ardhi ya Palestina.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina Riyad Al-Maliki amesema, viongozi wa Palestina wanakataa shinikizo lolote la Marekani kwa Umoja wa Mataifa na mashirika yake.

Pia ameongeza kuwa wizara yake inajitahidi kuandaa mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk.