Rais wa Tanzania atoa msamaha kwa wafungwa 1,631 katika wakati wa kusherehekea miaka 61 ya Uhuru
2022-12-12 08:56:26| CRI

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 1,60031 katika wakati wa kusherehekea miaka 61 ya uhuru wa nchi hiyo.

Katika taarifa yake iliyotolewa jumamosi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Hamad Msauni amesema, waliopata  msamaha huo ni pamoja na wanawake waliokuwa wanajawazito wakati wakihukumiwa kwenda jela, na wafungwa wengine wenye magonjwa sugu waliothibitishwa na jopo la madaktari chini ya usimamizi wa wakuu wa wilaya ama mikoa, na wafungwa wenye umri wa zaidi ya miaka 70. Wafungwa wengine watakaonufaika na msamaha huo ni wanawake wanaonyonyesha na wafungwa wenye ulemavu.

Hata hivyo taarifa hiyo imesema, wafungwa waliohukumiwa kwa kosa la kuwapa ujauzito wanafunzi wa kike na uhalifu wa kijinsia hawatapata  msamaha huo.