Zaidi ya wajasiriamali 300 wa Tanzania washiriki kwenye Maonyesho ya Biashara ya EAC
2022-12-12 08:57:23| CRI

Zaidi ya wajasiriamali 300 kutoka Tanzania wanashiriki kwenye  Maonyesho ya 22 ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) yanayohusu Biashara ya Viwanda Vidogo, vya ukubwa wa Kati na Vikubwa yaliyoanza rasmi Alhamis iliyopita mjini Kampala, Uganda.

Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema, Watanzania hao ni miongoni mwa washiriki 1,500 wa maonyesho hayo kutoka nchi wanachama wa EAC ambazo ni Burundi, Rwanda, Tanzania, Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Sudan Kusini.

Taarifa hiyo pia imesema, wajasiriamali kutoka Tanzania wataonyesha bidhaa zao za baharini, kilimo, utalii, bidhaa za ngozi na dawa za mitishamba.