Tume ya AU yaahidi kuendeleza juhudi za kuleta utulivu nchini Somalia
2022-12-13 08:48:55| CRI

Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imerejea tena ahadi yake ya kutimiza jukumu lake la kuunga mkono mchakato wa amani na utulivu nchini Somalia.

Mjumbe maalum wa Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika kuhusu Somalia Mohammed El-Amine Souef amesema, Tume ya Umoja huo itafanya kazi kwa karibu na wenzi wake kuleta amani nchini Somalia , nchi ambayo imekuwa ikipambana na waasi wa kundi la al-Shabab.

Pia ameahidi kufanya kazi kwa karibu na wenzi wote ili kuunga mkono juhudi za ujenzi mpya na maendeleo ya Somalia kwa ajili ya watu wa nchi hiyo.