Afrika Kusini yaimarisha zaidi uhusiano wa BRICS
2022-12-13 08:50:11| CRI

Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Naledi Pandor amesema, nchi hiyo inalenga kuimarisha zaidi uhusiano wa BRICS wakati ikichukua uenyekiti wa kundi hilo mwezi Januari, mwaka 2023, kutoka kwa China.

Waziri Pandor amesema, lengo kubwa la ushiriki wa Afrika Kusini katika kundi la BRICS ni kuimarisha ukuaji na maendeleo ya baadaye ya Afrika Kusini na kuimarisha maingiliano na uhusiano wa nchi wanachama wa kundi hilo pamoja na ushirikiano wa kunufaishana.

Amesema Afrika Kusini itaendelea kusisitiza ushirikiano halisi unaochangia moja kwa moja na kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa vipaumbele kwa ajili ya Afrika Kusini iliyo bora, Afrika iliyo bora na dunia bora kupitia uhusiano wake na wahusika wakuu katika masuala yanayohusiana na utawala wa dunia na mageuzi na maendeleo yake.