Walinda amani wa UM washirikiana na vikosi vya Afrika ya Kati kukabiliana na mashambulizi ya waasi
2022-12-13 08:54:58| CRI

Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema, askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wameshirikiana na vikosi vya Afrika ya Kati kuzuia mashambulizi yaliyofanywa na makundi ya waasi karibu na kituo cha msingi cha muda kilichoko karibu na eneo la Bambari, wilaya ya Ouaka.

Bw. Haq amesema, hakuna askari wa kulinda amani wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati waliojeruhiwa katika mapambano hayo.

Ameongeza kuwa, katika mashambulizi yaliyotokea mwishoni mwa wiki, gari moja la Umoja wa Mataifa lililokuwa karibu na kituo hicho lilishambuliwa kwa risasi mara kadhaa.