Rais wa China asisitiza ulinzi wa urithi wa utamaduni usioshikika
2022-12-13 08:57:28| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa ulinzi wa urithi wa utamaduni usioshikika na kuuonesha kwa dunia.

Rais Xi amesema hayo hivi karibuni alipotoa maagizo muhimu kuhusu ulinzi wa urithi wa utamaduni usioshikika. Pia amesema kuorodheshwa kwa “mbinu za jadi za utengenezaji wa chai na mila na desturi zinazohusika kijamii za China” kwenye Urithi wa Utamaduni Usioshikika wa Binadamu wa UNESCO kuna umuhimu mkubwa katika kukuza utamaduni wa chai wa China.