Kiongozi wa Sudan asisitiza umakini katika kuimarisha ushirikiano na China
2022-12-13 08:51:30| CRI

Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Utawala wa Sudan Abedl Fatah Al-Burhan amesisitiza utayari wa nchi hiyo kuboresha ushirikiano na China katika nyanja zote.

Taarifa iliyotolewa na Baraza hilo imesema, Al-Burhan amesema hayo Ikulu nchini Sudan alipokutana na Balozi wa China nchini Sudan Ma Xinmin, ambaye amemaliza muda wake, na kumkabidhi Balozi Ma Hati ya Juu ya Al-Neelain, kutokana na kutambua juhudi zake katika kuimarisha uhusiano wa pande mbili kati ya Sudan na China.

Kwa upande wake, Balozi Ma ameeleza kuridhishwa na uungaji mkono wa Bw. Al-Burhan na ushirikiano wa taasisi za serikali za Sudan na watu wake, ambavyo vilimwezesha kutekeleza majukumu yake kikamilifu.