Kenya na ITC zashirikiana kukuza mauzo ya nje
2022-12-14 10:07:01| CRI

Shirika la Kukuza Usafirishaji Bidhaa na Chapa la Kenya (KEPROBA) na Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC) jana zilisaini makubaliano ya ushirikiano ambayo yanalenga kuimarisha mauzo ya nje ya Kenya.

Mkurugenzi Mtendaji wa KEPROBA Bw. Wilfred Marube amewaambia wanahabari kwamba ushirikiano huo utawawezesha wauzaji bidhaa kutoka Kenya kuorodhesha bidhaa zao kwenye majukwaa ya kimataifa ya biashara ya mtandaoni ili kuimarisha mwonekano wa bidhaa za Kenya duniani.