WFP kushirikiana na Tanzania katika kuboresha mradi wa vyakula shuleni ili kukabiliana na utapiamlo
2022-12-14 10:10:13| CRI

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesaini makubaliano ya awali na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini Tanzania (TARI) yanayolenga kuboresha mradi wa utoaji wa chakula shuleni ili kukabiliana na utapiamlo.

Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imesema, chini ya mradi huo, mashamba ya shule yataanzishwa katika shule 50 za msingi mkoani Kigoma kwa lengo la kuboresha utoaji wa chakula shuleni kama mfumo wa ulinzi wa jamii kukabiliana na utapiamlo, hususan upungufu wa lishe muhimu kati ya watoto wanaoenda shule na vijana.

Taarifa hiyo pia imesema, mradi huo utaongeza uzalishaji na matumizi ya mahindi na maharagwe yaliyoongezwa lishe, matunda, na mboga za majani katika siku za shule, huku ukichangia katika kuboresha matokeo ya elimu katika shule zililolengwa.