China yatumai jamii ya kimataifa ichukue vitendo halisi kuzisaidia nchi za Afrika
2022-12-14 10:08:41| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema, China inatumai kuwa jamii ya kimataifa itashughulika na mahitaji halisi ya nchi za Afrika kwa kuchukua vitendo halisi na kusaidia katika maendeleo ya uchumi na jamii na ustawi wa watu wa bara hilo.

Wang amesema hayo alipojibu swali na wanahabari kuhusu ripoti ya hivi karibuni kuhusu diplomasia ya kimabavu ya Marekani barani Afrika, ambayo inadai kuwa, ushiriki wa Marekani barani Afrika unalenga kupunguza ushawishi wa China na Russia katika bara hilo na dunia, na wala si kuchukua hatua halisi katika kukabiliana na changamoto za maendeleo barani Afrika.

Wang amesema, ripoti hiyo iliyotolewa na taasisi muhimu ya Afrika, inatoa mtazamo wa Afrika katika uhusiano kati ya bara hilo na Marekani.