Mvua kubwa yasababisha vifo vya zaidi ya watu 141 nchini DRC
2022-12-14 10:06:10| CRI

Idara ya afya za umma ya Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) jana imesema, watu zaidi ya 141 wamefariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo kadhaa kuanzia Jumatatu usiku hadi mapema Jumanne.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, familia 38,787 zilikumbwa na mafuriko na nyumba 280 kubomolewa.