Shirika la hisani laonya juu ya utapiamlo mkali nchini Somalia
2022-12-16 07:58:50| CRI


 

Naibu mkurugenzi wa Shirika la hisani la Save the Children of Somalia, Binyam Gebru amesema, zaidi ya watoto 500,000 nchini humo wanatarajiwa kukabiliwa na utapiamlo mkali itakapofika mwezi April mwakani kutokana na ukame mkali, bei kubwa ya vyakula, mapigano na magonjwa.

Katika taarifa yake iliyotolewa mjini Mogadishu jana jumatano, Gebru amesema mamilioni ya watoto wanakabiliwa na utapiamlo, magonjwa makali na vifo.

Taarifa hiyo imekuja siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kutabiri kuwa nusu ya watu wanatarajiwa kukabiliwa na njaa kali itakapofika mwezi April mwakani, ikiwa ni pamoja na watoto milioni 1.8 watakaokabiliwa na utapiamlo mkali, na wengine 513,500 watakaokumbwa na utapiamlo mbaya.