Lawama dhidi ya sera ya kibiashara ya Marekani yaonesha maoni ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa
2022-12-16 09:12:34| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema, pande mbalimbali za Shirika la Biashara Duniani (WTO) zimepinga vitendo vya Marekani vya upande mmoja na vya kujilinda kibiashara, ikionesha maoni ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.

Jumatano wiki hii mjini Geneva, WTO iliitisha mkutano, ambapo China, Umoja wa Ulaya, Russia na nchi wanachama wengine zililaani vitendo vya Marekani vya kuvuruga mnyororo wa uzalishaji duniani.

Wang amesema Marekani inadai ushindani wa haki kwa sauti kubwa, lakini wakati huohuo inatoa ruzuku kubwa yenye ubaguzi, ili kusaidia kampuni zake kupata uwezo zaidi wa ushindani.