China yasema maoni ya nchi za Afrika na watu wake yanastahili kuthaminiwa
2022-12-16 08:02:31| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema, maoni ya nchi na watu wa Afrika yana ushawishi zaidi kuhusu nani anaifaa zaidi Afrika.

Wang amesema hayo alipojibu kauli za maofisa wa Marekani walioshiriki katika Mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika uliofunguliwa mjini Washington, kwamba vitendo vya siri vya China vitaharibu utulivu wa Afrika, na Marekani ni mshirika wa kwanza anayezifaa nchi za Afrika.

Akizungumzia kauli hiyo, Wang amesema kusaidia maendeleo ya Afrika ni jukumu la pamoja la Jumuiya ya Kimataifa, na China inaikaribisha kujumuiya ya kimataifa ikiwemo Marekani kuongeza uwekezaji na kufanya ushirikiano wa kunufaishana na Afrika.

Pia amesisitiza kuwa, China inatumai kuwa Marekani itatendea ushirikiano kati ya China na Afrika kwa njia iliyo wazi, na kwamba nchi za Afrika na watu wake wana hekima na uwezo wa kuchagua washirika wanaoendana na maslahi yao.