Uingereza yahimizwa kuacha mchezo wa kisiasa katika shambulizi dhidi ya ubalozi wa China
2022-12-16 09:11:56| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin ameihimiza Uingereza kufuata sheria husika za kimataifa na kutekeleza majukumu ya kidiplomasia ya pande mbili, kuheshimu kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa, na kuacha michezo ya kisiasa, ili kuuwezesha kihalisi ubalozi wa China nchini humo kutekeleza majukumu yake ya kawaida.

Wang ameyasema hayo alipoulizwa na wanahabari kuhusu tukio la shambulizi dhidi ya ubalozi mdogo wa China huko Manchester nchini Uingereza lililotokea tarehe 16 Oktoba, ambapo waandamanaji waliingia kwenye ubalozi huo kwa njia haramu, na kuwashambulia wanadiplomasia.

Wang amesema, Uingereza haikuiarifu China kuhusu maandamano hayo, haikutekeleza jukumu lake la kulinda ubalozi wa China, na badala yake, ilipaka matope China na kulinda wahalifu, kitendo ambacho kimepuuza kanuni na sheria, na hakikubaliki kamwe na China.