Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa asikitishwa na vifo vilivyotokana na mafuriko nchini DRC
2022-12-16 08:01:45| CRI

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric jana amesema, katibu mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres ameeleza kusikitishwa kwake na vifo vya watu na uharibifu mkubwa wa mali uliosababishwa na mafuriko yanayoikumba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tangu mwaka 2019.

Msemaji huyo amesema, Bw. Guterres ametoa rambirambi zake kwa familia za wahanga, pamoja na serikali na watu wa DRC.