Mashirika ya biashara ya Afrika yaungana kukuza biashara
2022-12-16 09:08:58| CRI

Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) jana lilisaini makubaliano ya awali na Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda cha Abuja (ACCI) cha Nigeria ili kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya mashariki na magharibi mwa Afrika.

Akizungumza katika hafla hiyo, rais wa ACCI Bw. Al-Mujtaba Abubakar alisema, ushirikiano huo utaongeza ubadilishanaji wa taarifa za kibiashara, taarifa za wateja na kutoa jukwaa la utatuzi mbadala wa migogoro katika masuala ya biashara.