Rais wa China ahutubia ufunguzi wa kikao cha COP15
2022-12-16 09:06:33| CRI

Rais wa China Xi Jinping jana alhamis alihutubia kwa njia ya video hafla ya ufunguzi wa kikao cha pili cha ngazi ya juu cha Pande Zilizosaini Mkataba wa Viumbe Anuwai (COP15) unaofanyika mjini Montreal, Canada.

Katika hotuba yake, rais Xi amesema mshikamano na ushirikiano ni njia pekee ya ufanisi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali duniani, kutokana na kwamba binadamu wanaishi katika jamii yenye mustakabali wa pamoja.

Amesema mfumo wa ikolojia ulio thabiti ni muhimu kwa ustawi wa binadamu, na ni lazima kufanya kazi kwa pamoja ili kuboresha ustawi na masikilizano kati ya binadamu na asili, kujenga jamii ya viumbe vyote duniani, na kujenga dunia nzuri na safi kwa ajili ya wote.

Rais Xi pia amesema katika hotuba yake kuwa, China imefanya juhudi halisi ili kuboresha maendeleo ya ikolojia na ulinzi wa viumbe hai, na kuongeza kuwa anuwai ya viumbe, utulivu na uendelevu wa mfumo wa ikolojia vimeendelea kuboreshwa.

Amesema China itajitahidi kuunga mkono na kutoa msaada kwa nchi nyingine zinazoendelea kupitia Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, Muungano wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kijani na Mfumo wa Viumbe Hai wa Kunming, ili kuimarisha usimamisi wa viumbe hai duniani ufikie kwenye ngazi mpya.