ECOWAS yaahidi ushirikiano ili kuhakikisha uchaguzi wa amani na haki nchini Nigeria
2022-12-16 08:00:15| CRI

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imeahidi kushirikiana na wadau wa kisiasa wa Nigeria ili kuhakikisha uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Februari mwakani utafanyika kwa amani na haki.

Taarifa ya ECOWAS iliyotolewa jana imesema, mgogoro unaotokana na uchaguzi umekuwa chanzo cha vurugu katika eneo la Afrika magharibi, na ushawishi wa kisiasa na mivutano kati ya jamii mara nyingi ikichochea vurugu hizo.

Habari zinasema, Nigeria itafanya uchaguzi mkuu tarehe 25, Februari, 2023 kuchagua rais na wabunge.