China yafanya utafiti kuhusu watu walio hatarini zaidi kuwa na dalili mbaya za maambukizi ya COVID-19
2022-12-16 09:07:20| CRI

Tume ya Taifa ya Afya nchini China (NHC) imesema inafanya utafiti ili kugundua watu walio hatarini zaidi kuwa na hali mbaya baada ya kuambukizwa virusi vya Corona, ikiwemo wazee na wale wenye magonjwa sugu.

Hatua hiyo inafuatia China kutoa kipaumbele zaidi kwenye matibabu badala ya kudhibiti maambukizi, na juhudi zaidi kutolewa katika ulinzi wa makundi yaliyo hatarini na kuboresha huduma za afya ya msingi.

Mkuu wa Idara ya Afya ya Msingi katika Tume hiyo Nie Chunlei amesema, maeneo yote yametakiwa kuwa na uelewa kamili wa afya ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65, hususan wale wenye magonjwa sugu kama ugonjwa wa moyo, kiharusi na shinikizo la damu. Ameongeza kuwa, wazee hao wanaweza kuwekwa katika makundi tofauti kutokana na magonjwa waliyo nayo, umri, na hali ya chanjo ya COVID-19.