Watanzania milioni 10 kupata huduma bora ya maji chini ya ufadhili mpya wa WB
2022-12-16 09:08:21| CRI

Watanzania milioni 10 wanatarajiwa kupata huduma bora ya maji na wengine milioni tisa kupata miundombinu bora ya vyoo kupitia ufadhili kutoka Benki ya Dunia.

Katika taarifa yake, Benki ya Dunia imesema ufadhili huo mpya utasaidia upanuzi wa mradi huo kutoka wilaya 86 katika mikoa 17 hadi wilaya 137 katika mikoa 25 nchini Tanzania. Pia taarifa hiyo imesema, mradi huo utawezesha shule za msingi 1,850 za umma na vituo 2,600 vya afya kufikiwa na mindombinu bora na ya kisasa ya afya.