Wachina wanaoishi nchini Kenya watoa msaada wa chakula kwa waathirika wa ukame
2022-12-19 09:02:02| CRI

Jumuiya ya wachina wanaoishi nchini Kenya wametoa zaidi ya tani 60 za msaada wa chakula kwa waathirika wa maafa ya ukame nchini humo, ili kuwasaidia kupita kwenye wakati mgumu.

Akiongea kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo, mkurugenzi wa ofisi ya naibu rais wa Kenya George Mcgoye amepongeza msaada huo wa hisani na kusema utasaidia maelfu ya familia zilizoathiriwa na maafa, na kutoa shukrani zake kwa uungaji mkono endelevu wa jumuiya ya wachina na Ubalozi wa China kwa Kenya.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa wiki iliyopita na Idara ya usimamizi wa ukame ya Kenya, hivi sasa idadi ya watu wanaohitaji misaada ya kibinadamu nchini humo imefikia milioni 4.35, na watu wapatao milioni moja wanakabiliwa na utapiamlo mkali.