Matumizi ya SGR nchini Kenya yamefikia kiwango kipya kabla ya msimu wa sikukuu
2022-12-20 09:04:25| CRI

Takwimu zilizotolewa jana na serikali ya Kenya zinaonesha kuwa treni ya reli ya SGR ya Kenya ilibeba abiria milioni 1.74 katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka huu, zikiwa ni ongezeko la robo ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS) imesema kuwa abiria milioni 1.74 ni ongezeko la asilimia 28 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka wa 2021, wakati treni hiyo ilisafirisha watu milioni 1.35. Mwaka 2021 treni hiyo ilisafirisha karibu watu milioni 2. Hii ina maana kuwa kwa idadi ya watu ya milioni 1.74 ya hadi kufikia mwezi Septemba, matumizi ya SGR kwa mwaka wa 2022 yatafikia kiwango kipya huku safari za kabla ya msimu wa sikukuu zikiongezeka.

Jumatatu huduma ya mauzo ya tiketi ilionesha kuwa tiketi za kuanzia Desemba 20 hadi Desemba 27 zimeuzwa, huku abiria wengi wakiwa watamiminikia Mombasa kwa ajili ya sikukuu ya Krismasi.