Watu watano wafariki katika ajali ya kuporomoka kwa jengo nchini Tanzania
2022-12-20 09:07:21| CRI

Mkuu wa wilaya ya Moshi, mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania Bw. Abbas Kayanda amesema wafanyakazi watano wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa baada ya jengo la ghorofa mbili linaloendelea kujengwa kuporomoka saa 3 usiku wa Jumapili wilayani humo.

Bw. Kayanda alisema kulikuwa na wafanyakazi wa ujenzi 30 katika eneo la ajali hiyo, na 16 kati yao waliokolewa bila kujeruhiwa. Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa ajali hiyo imesababishwa na kiwango kibaya cha ujenzi.