Rais Xi asisitiza kuwa na ukurasa mpya katika utekelezaji wa Katiba ya China katika zama mpya
2022-12-20 09:05:15| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwekwa ukurasa mpya katika utekelezaji wa Katiba ya China katika zama mpya, wakati China inaadhimisha miaka 40 ya kupitishwa kwa Katiba yake ya sasa. Rais Xi amesema jitihada zinahitajika ili kuongeza uelewa kuhusu Katiba, kuendeleza msingi wa Katiba, kuendeleza utekelezwaji wa Katiba, na kutumia vyema nafasi yake muhimu katika utawala wa nchi. Kwenye makala maalum iliyotolewa jana, Rais Xi amesema kwa kufanya hivyo, dhamana thabiti inaweza kutolewa kwa ajili ya kuijenga China kuwa nchi ya kijamaa ya kisasa kwa pande zote, na kuendeleza taifa la China katika nyanja zote.

Pia amesema utungaji wa sheria na utekelezaji wa Katiba, vinaashiria maendeleo ya ustaarabu wa binadamu na kusisitiza uboreshaji wa jamii ya binadamu.